Monday 18 August 2014

HAKUNA AWEZAYE KUZUIA MPANGO WA MUNGU JUU YA MAISHA YAKO

HAKUNA AWEZAYE KUZUIA MPANGO WA MUNGU JUU YA MAISHA YAKO
Tuanze kwa kusoma Ayubu(Job 42:2) Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Haya yalikuwa ni maneno ya Ayubu mcha Mungu baada ya kupitia majaribu mengi ambayo yalisababisha majeraha na maumivu makubwa katika maisha yake. Pamoja na misukosuko aliyoipitia Ayubu alisimama imara katika imani yake na kuzidi kumtumaini Mungu katika yote aliyoyapitia. Wapo ndugu na jamaa zake wa karibu sana akiwepo mke wake mpendwa ambao kutokana na mateso ambayo Ayubu aliyapata waliona ushauri pekee ambao ulimfaa Ayubu ilikuwa ni kuacha kumtumainia/kumcha Mungu. Katika kitabu cha Ayubu 2:9 bibilia inasema Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe. Hii ni kauli inayoashiria kukata tamaa (yaani kukosa tumaini). Hata hivyo kwa kuwa Imani ya Ayubu kwa Mungu ilikuwa kubwa mno, Ayubu kamwe hakuacha kumtumainia Mungu na hatimaye alipata ushindi.  Mwisho kabsa tunaona jinsi ayubu alivyobarikiwa kwa Baraka zilizokuwa ni kuu mno.  Katika Ayubu 42:12 bibilia inaandika kuwa Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu, na punda wake elfu.
Yawezekana nawewe mtu wa Mungu unapitia katika magumu ambayo kwa namna moja ama nyingne yameleta majeraha makubwa katika maisha yako. Ndugu ,jamaa na na rafki zako wa karibu uliowategemea wamekudharau na wamekuona huna msaada wowote katika maisha yao. Wapo wanaokusengenya na wanaokusimanga kila kuitwapo leo na yawezekana umekata tama hata ya kuishi. Amini nakuambia kwa kuwa Mungu amekupa fursa ya kuwa hai mpaka leo na saa hii, tambua kuwa Mungu ana makusudi mema nawewe.   Hayo unayoyapitia unayoyaona kwako yamekuwa ni mzigo usioweza kuubeba kesho yatageuzwa na kuwa mtaji wako wa kufanikiwa milele.
Ni wangapi ambao waliomcheka, kumdhihiki na kumtukana Ayubu kwa aliyopitia lakini baadaye walimwangukia?. Haijalishi ni wangapi waliokuzunguka wakikudhihaki na kukucheka kutokana nay ale unayoyapitia, ipo siko watakuangukia.  Wanaodhani kuwa kwa kuwa wao wamefanikiwa kwasababu tu wamesoma sana na wewe walikuacha vidato vya nyuma ipo siku watakuja kuomba kazi kwako.  Kwani ni wangapi ambao hata kidato cha tano na sita hawajafika lakini leo wana masters.  Binafsi nimejifunza kitu cha msingi kutokana na maisha ya Harith Kapiga ambaye ni mtangazaji wa Clouds fm, MC na mchungaji ambaye anasema hajawahi soma kidato cha tano wala sita lakini kwa sasa ana Masters.  Ninaamini hata wewe unaweza kufika mahali pale Mungu alipokusudia iwapo tu utaamua kusimama imara mahali ulipo pasipo kusikiliza mawazo na maneno ya wanao kukatisha tamaa.
Wema na fadhili za Mungu ziambatane  nawewe siku zote za maisha yako.
Mwandishi: Patson Mbewa.


1 comment:

faigonmacdiarmid said...

SEGA Genesis (Mega Drive) Games: 569 Words - Choegomachine
Play all our SEGA Genesis (Mega Drive) games online in 2019 SEGA Master System / Genesis Model 카지노 A / 파라오카지노 Mega Flashback. Genesis / Model A.