KILIMO BORA CHA
VITUNGUU MAJI
Vitunguu ni mojawapo ya
zo muhimu ambalo hulimwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi Tanzania. Zao la
vitunguu hulimwa kama zao la bishara katika maeneo mbalimbali nchini na
huwapatia watu kipato kikubwa ambacho huwasadia katika kutatua changamoto
mbalimbali za kiuchumi na kusaidia katika kupambana na umasikini.
Vitunguu hutumika kama
kiungo muhimu cha kuongeza harufu nzuri na ladha katika vyakula. Hutumika katika utengenezaji wa supu, siki
,kachumbari nk. Majani ya vitunguu yana madini ya chokaa na wanga kwa wingi.
Vilevile virutubisho vingine kama protini, chuma na ascorbic acidi hupatikana
katika vitunguu.
Nchini mwetu vitunguu hulimwa kwa wingi katika mikoa
ya Tanga, Arusha sehemu za Mang’ora na
Babati, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa
mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha , Mara , Morogoro wilayani
Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo ,Mbeya Kilimanjaro na baadhi ya sehemu za
Mkoa wa Singida.
Katika shamba lililo
hudumiwa vizuri na kupandwa katika hali ya hewa na aina ya mbengu. Vitunguu
hutoa kiasi cha tani (10) hadi 16 kwa ekari moja.
Mazingira
Vitunguu husitawi vizuri katika maeneo yenye miinuko
kuanzia mita 800 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari. Hupendelea hali ya ubaridi
kiasi hususani wakati wa kuotesha mbegu kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa
kwa miche iliyoko kwenye kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 27°C. Joto la juu
hufanikisha utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji. Hivyo ni vema vitunguu
vioteshwe wakati wa baridi ili viweze kuvunwa wakati wa Joto.
Udongo:
Huhitaji udongo tifutifu wenye rutuba
nyingi usiotuamisha maji na usiopasukapasuka. Huhitai udongo ulio katika kipimo
cha pH kati ya 6.0 na 7.0
Aina za vitunguu vinavyoshauriwa kuoteshwa katika ukanda wa Joto ni
Red Creole, Texas Grano, Tropical Red F1 hybrid, Singida local na Pretoria
Grano.
Baadhi ya aina ya vitunguu na sifa zake
Aina
|
Siku
za
kukomaa
|
Umbile
la kitunguu
|
Rangi
ya
ganda
|
Rangi
ya
ndani
|
Red
Creole
|
150
|
Nusu bapa
|
Nyekundu
|
Nyekundu kahawia
|
Red
Bombay
|
160
|
Duara
|
Nyekundu angavu
|
Nyekundu kahawia
|
Texas
Grano
|
165
|
Duara
|
Njano (kaki)
|
Nyeupe
|
Upandaji
na Uoteshaji miche
Mbegu za vitunguu huoteshwa kwanza kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri
takribani wiki mbili. Vitunguu maji huoteshwa zaidi kwa
kutumia mbegu kwenye kitalu na kisha kupandikizwa shambani.
Kabla
ya kuzipanda mbegu. Tengeneza
tuta lenye upana wa mita moja (sentimeta 100) na urefu wowote kutokana na
mahitaji yako. Weka mbolea aina ya
samadi kiasi cha ndoo moja ukiichanganya vizuri na udongo kwa kila mita ya
mraba moja.
Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa miche ya kutosha
kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba. Mwagilia kitalu kwa maji ya kutosha
siku moja kabla ya kupanda mbegu.
Panda
mbegu katika misitari yenye nafasi ya sentimita10 hadi 15 kutoka msitari hadi
msitari Na kina cha sentimita moja kwa kumiminwa polepole kwenye mistari/mifereji
iliyoandaliwa vizuri. Kisha fukia kwa kunyunyuzia udongo juu ya mbegu zilizoko
kwenye mifereji.
Weka
matandazo kisha mwagilia mara mbili kila siku(asubuhi na Jioni) hadi mbegu
zitakapoota.Mbegu bora huota baada ya
siku 7 hadi 12 kutegema hali ya hewa. Mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka
siku 21 udongo unapokuwa wa baridi sana na hali ya hewa ikiwa nzuri, mbegu
huota mapema zaidi, hata ndani ya siku 4.
Kuandaa
shamba
Tayarisha shamba
vizuri mwezi mmoja kabla ya kupandikiza. Udongo utifuliwe vizuri kwenye urefu
kina cha sentimita 30 na ulainishwe vizuri na majani yaondolewe kabisa. Mbolea
za asili ziwekwe shambani ili kuufanya udongo ushikamane vizuri na uweze
kuhifadhi mbegu. .Kisha tengeneza matuta au majaruba kufuatana na nafasi za
kupandia ili kurahisisha umwagiliaji.
Kupandikiza vitunguu shambani
Miche huwa
tayari kupandikizwa shambani wiki 6 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche iliyo
tayari huwa na urefu wa sentimita 12 hadi 15 na unene 1/2 au 3/4 ya kalamu ya
risasi kwenye shina.
Kabla ya kupandikiza loanisha kitalu ili kuepuka
kukata mizizi. Ng’oa miche kwa kutumia kijiti au chombo kingne na punguza
majani na mizizi ili kusaidia kuzuia upotevu wa maji. Wakati wa upandikizaji
chagua miche iliyo na afya nzuri ambayo haikushambuliwa na magonjwa na wadudu.
Miche ipandwe wakati wa asubuhi na jioni ili kuepuka jua na joto kali
linaloweza kuidhoofisha miche. Miche ipandikizwe kwenye nafasi ya upana wa
sentimita 20 hadi 30 na nafasi ndani ya mstari ni sentimita 10 hadi 15. Baada
ya kupandikiza mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka miche itakapo
shika vizuri.
UTUNZAJI
WA SHAMBA
A).
Mbolea
Vitunguu vina
hitaji udongo wenye rutuba ya kutosha ili viweze kusitawi vizuri.mbolea za
kukuzia kama vile CAN au S/A ziwekwe shambani wiki 3 na ya 6 baada ya
kupandikiza. Kiasi cha mifuko 3 au 4 kinatosha kuwekwa kwenye shamba la ukubwa
wa hecta moja. Mbolea iwekwe katika kiwango sahihi yaani kifuniko kimoja cha
soda (gram 5) kwa mche. Mbolea iwekwe kwenye mistari bila kugusa mche.
Upungufu wa
kirutubisho cha Nitrojeni unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa
kitunguu. Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa kitunguu na
unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora.
B). Umwagiliaji:
Ili kupata mavuno bora shamba linatakiwa kuwa na
maji ya kutosha kila wakati. Umwagiliaji wa maji yanayokwenda chini kiasi cha
sentimeta moja (1cm) au zaidi kwa wiki ni mzuri kwa kupata vitunguu vikubwa.
Epuka umwagiliaji kupita kiasi au pungufu kwani hali hii huweza kusababisha
mipasuko. Punguza kumwagilia wakati vitunguu vinapokomaa kwani husababisha
vitunguu vinavyokomaa kuoza.
C).
PALIZI (UTHIBITI WA MAGUGU)
Magugu yaondolewe mara kwa mara kila
yanapojitokeza hasa miche inapokuwa michanga.
Ukuaji na mavuno yanaathirika sana endapo magugu hayatadhibitiwa mapema.
Magugu yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe dogo la mkono. Wakati
mwingine ni mchanganyiko wa madawa, jembe la mkono na kungolea kwa mkono.
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
A). MAGONJWA
i.
Ubwiri vinyoya juu(powdery mildew)
na wa chini (Downy mildew)
Huu husababishwa na ukungu
na hupendelea hali ya unyevu nyevu. Hushambulia hushambulia majani ya mimea iliyo shamabani na
hata miche michanga. Dalili zake Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa kwenye
majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe unatokea na kuongezeka kwa haraka
kwenye sehemu au nyakati za baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya
vitunguu na huweza kupeperushwa mbali na upepo.
Nyunyuzia dawa mojawapo zifuatazo kuzuia ukungu: - Dithane-M45,
Ridomil, Topsin M70 na Cupric Hydroxide (Champion).
ii.
Ugonjwa wa doa la pinki (Purple
blotch)
Huu nao ni ugonjwa uletwao na Ukungu na hushambulia
majani, shingo na vitunguu vilivyokomaa. Huanza kama doa dogo linalozama ndani
ya jani na kisha linaongezeka ukubwa na kufanya baka la rangi ya Zambarau
ambalo huonekana katikati ya jani ambalo baadaye huwa jeusi. Shina
lililoshambuliwa hulegea na kuanguka katika wiki ya tatu au ya nne baada ya
dalili za ugonjwa kuonekana. Vitunguu vilivyokomaa huoza kuanzia shingoni na
hugeuka rangi kuwa ya njano iliyochanganyika na nyekundu.
Zuia ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:-
- Kupanda aina ya vitunguu visivyoshambuliwazidi na ugonjwa huu (Red Creole)
- Kubadilisha mazao
- Vuna vitunguu kwa wakati sahihi
- Matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu.
- Kwa upande mwingine,matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu uongeza mlipuko wa magonjwa.
- Viatilifu kama vile Mancozeb Dithane-M45, Ridomil, Topsin M70 na Cupric Hydroxide (Champion).
i.
Kuoza kwa shingo (Neckrot)
Husababishwa na ukungu na hupendelea vile vile hali ya unyevunyevu.
Hushambulia zaidi vitunguu vilivyohifadhiwa. Ugonjwa huu husababisha
vitunguu kuwa laini, hubonyea na huonekana kama vilivyopikwa. Huanzia kwenye
shingo na baadaye huenea kwenye kitunguu chote na kufunikwa na ukungu wa
kijivu.
Namna ya kuzuia:-
- Vuna vitunguu kwa wakati sahihi
- Kubadilisha mazao
- Tumia njia sahihi wakati wa kuvuna, epuka kuchubua au kukikwaruza wakati wa kuvuna
- Kausha vitunguu vizuri baada ya kuvuna
- Hifadhi vitunguu sehemu zisizo na unyevu mwingi
B). UDHIBITI WA WADUDU
Sata (Cutworms) Utitiri wa vitunguu (Onion thrips),
Funza wa vitunguu (Onion maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms), Bungua weupe (White grub), ni miongoni
mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.
Tumia dawa zilizothibitishwa na wataalamu.
Uvunaji
Vitunguu huwa tayari kuvunwa baada ya miezi mitatu
mpaka mitano (siku 90 mpaka 150) tangu kusia mbegu kutegemeana na aina na hali
ya hewa ya eneo husika. Kabla ya kuvuna mkulima anaweza kuanza maandalizi ya
kuvuna mwezi mmoja kabla kwa kuondoa udongo polepole kwenye kitunguu ili
kusidia ukaushaji mzuri. Vitunguu vianze kuvunwa pale ambapo asilimia 50 hadi
75 ya vitunguu huonesha kulegea au kunyauka. Vitunguu huvunwa kwa hung’olewa na
kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa na kuwekwa kwa ajili ya kukata
shingo. Mizizi pia inapunguzwa na vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa
kusafirishwa nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa.
KUHIFADHI
Vitunguu vilivyovunwa vikaushwe vizuri kabla ya
kuvihifadhi. Vihifadhiwe katika eneo lenye hewa ya kutosha, isiyokuwa na unyevu
wala jua kali. Vitutnguu vihifadhiwe kwa kuvitandaza juu ya chanja au kwa
kufunga mashina yake yaliyokauka vizuri kwa kuyaning’iniza sehemu ya
kuhifadhia. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au zaidi bila
kuharibika.
Mavuno
Mavuno ya
vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Vitunguu pia
hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu
vinaweza kutoa mavuno kati ya tani 30 hadi 40 kwa hekta moja.
REJEAA
Dr MGEMBE. Onion Swahili brochure (Sokoine University of Agriculture (SUA))
The ministry of Agriculture, Food and Cooperative,
extension department (2002)
Kwa maoni au
ushauri na maswali wasiliana nami kwa (SMS au kwa kwa kupiga) namba zifuatazo:-
email: patsonjackson386@gmail.com
4 comments:
Habari kaka, mimi nataka kujikita na kilimo cha vitunguu, naomba msaada kuwa je ni muda gani naweza kuanza kulima viyunguu pia je ni kiasi cha gharama gani kwa heka moja ya kulima vitunguuu.
Akhsante
Salum Simba
Asante
ahsante kwa maelezo mazuri, napenda kujua kwa mkoa wa kilimanjaro wilaya ya moshi mjini vitunguu maji huanza kulimwa lini na mwisho kabisa wa kupanda ni mwezi gani
asante sana kwa somo zuri sasa ni kuingia shambani kwa vitendo naomba namba zako kama nahitaji msaada zaidi namba zangu ni 0757392133 ni muhimu
Post a Comment