Saturday 16 August 2014

UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI- WATERMELON PRODUCTION

UTANGULIZI
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.  Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga  inayotambaa.  Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama  matango,maboga na maskwash.  Zao la tikiti maji  ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa  na kuhudumiwa  vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.  Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua:  kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu  mpaka wa tisa.
UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.

UPANDAJI
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja  katika kila  shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi  na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo  katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati  mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.
MATANDAZO (MULCHES)
Matandazo ina maana ya kutumia  nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche  kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu  kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea za viwandani aina ya  NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana.  Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
UMWAGILIAJI
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache.  Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie  juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume  huwa  ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.  
Hii hufanywa kwa, kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.
                                                                       

                                             
                                                                               
MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama
Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.
 UVUNAJI MATIKITI
Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii  hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa  na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;
Ø Rangi ya mng’ao hupotea
Ø Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Ø  Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.
Ø  Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
Soko la matikiti maji
Ukubwa wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja limekuwa  likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti  dogo mpaka 3000  kwa tikiti kubwa katika masoko.

Mavuno
Mavuno ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti  pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya
TANI 15-36 kwa hekta moja

15 comments:

Timoth Stanslaus Chale said...

Asante sana mtoa elimu!, nimeridhika na elimu yako na itanisaidia sana!!, ila naomba tena ushauri wako, mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe Morogoro, ninasomea digrii ya biashara na maendeleo ya ujasiriamali, BBA-ED (BACHELOR OF BUSINESS ADMINISTRATION IN ENTREPRENEURSHIP DEVELOPMENT, SECOND YEAR). Nina plan ya kulima matikiti in medium scale, yaani natarajia kulima zaidi ya ekali 10. sasa naomba unisaidie kunipa ushari, ni mkoa gani na wilaya gani, itanifaa zaidi ili nifanikiwe kwa kiwango kinachotakiwa???,

James D Mnyema said...

Kaka kwa hapo Morogoro, matikiti maji hulimwa zaidi na kustawi vizuri maeneo ya TURIANI, KINGOLWIRA na MIKESE... nakushauri tembelea maeneo hayo utakutana na wakulima na kupata maelezo zaidi ya jinsi ya kupata mashamba nk...

combizzle said...

kwa ekari moja nahitaj kuwekeza kiasi gani na pia faida ni shillings ngapi? Pia mbegu gani bora zenye soko katika soko nchini? Unaweza nijibu kupitia 0787076204 au kwa email lewisbeatus@gmail.com

Anonymous said...

Asante kwa somo zuri mdau

Unknown said...

Asante kwa somo kaka

Unknown said...

Shukrani sana kwa somo zuri ndugu, naomba kama kuna group linalotoa elimu juu ya kilimo Add me +255675438353.

Unknown said...

Eka kumi nyingi. Anza kidogo. Kama unasoma Mzumbe Moro imetajwa kuwa eneo zuri kwa ajili ya matikiti

Unknown said...

Kwa kweli nimelifurahia somo BT napenda kujua mbegu IPI ni nzuri na makadirio acre moja inaweza kugharimu sh ngapi mpk kuvuna

Unknown said...

Kwa kweli nimelifurahia somo BT napenda kujua mbegu IPI ni nzuri na makadirio acre moja inaweza kugharimu sh ngapi mpk kuvuna

Unknown said...

Nimesoma vizuri sana na nimeelewa..nipo Tanga mjini naweza kufanya kilimo hiki nikafanikiwa kupata mavuno mazuri? Ahsante

Unknown said...

Nimesoma vizuri sana na nimeelewa..nipo Tanga mjini naweza kufanya kilimo hiki nikafanikiwa kupata mavuno mazuri? Ahsante

Eng. Leon said...

Mwalimu naomba ujibu madwali tafadhali

Unknown said...

asante kwa somo naomba kwa yeyote anayejua anijibu naweza panda tikiti septemba mbegu ya F1 kwa morogoro na yakatoka vizuri maana nahofia mvua mwenz wa 12 ambapo ndo itakuwa muda wa mavuno msaada plz wadau

Unknown said...

Asante kwanza somo zuri,
Namm Ni mdau wa kilimo cha tikiti,

Naomba niadd kwenye group last whatsapp Kimalo husika na kilimo kama itawezekana no yangu Ni 0766240826

Unknown said...

Gambling in Qatar - Casino & Sports Book
All the website to buy jordan 18 white royal blue latest casino games and great air jordan 18 retro varsity red sports betting odds. show to get air jordan 18 retro red Sports betting, gambling on football, eSports, poker and air jordan 18 retro racer blue shipping more. 프리 벳 Visit our website.