UTANGULIZI
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani
zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za
kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi
kwenye matumizi. Matikiti maji ni
mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa.
Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama
kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa
sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika shamba la ukubwa wa shamba
la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa
vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia
katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
HALI YA HEWA
Mimea
hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto
kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya
fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti
hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30
sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa
katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua: kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi
cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa
magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri
ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji
udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali
na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa
mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
MAENEO YANAYOFAA
KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda
wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani
ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi
wa tatu mpaka wa tisa.
UANDAAJI WA
SHAMBA
Kabla
ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha
ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.
UPANDAJI
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha
mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila
shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu
sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa
kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30
kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia
kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid)
ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora
wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni
kizazi cha pili (F2)
UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea ya michikichi huanza kuota,
baada ya kama wiki 2. Hivyo katika Mbegu mbili
ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.
Aangalizo using’oe mche
bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia
kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya
kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza
rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia,
ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.
Wakati
mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni
lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.
MATANDAZO (MULCHES)
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na
mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo
(mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu
vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo
yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko
wa udongo.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea za viwandani aina ya NPK au
mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni
midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana. Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea
ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na
potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
UMWAGILIAJI
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara
wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii
huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na
siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji
kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya
wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo; usimwagilie matikiti
wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani
kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join
kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa
uchavushaji.
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni
madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa
zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji
kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na
iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.
Hii hufanywa kwa, kukata
maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo
kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee
kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi.
Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.
MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia
majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi
ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine
yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za
magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na
pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza
kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti
hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia
kuua wadudu wa majani, maua na matunda.
UVUNAJI MATIKITI
Kabla ya
kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi
mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti
lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake
huwa kama ifuatavyo;
Ø Rangi
ya mng’ao hupotea
Ø Upande
wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Ø Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na
kuwa kijivu.
Ø Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na
kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna
matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa
matumizi binafsi
Soko
la matikiti maji
Ukubwa
wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti
madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi
wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa
miaka kadhaa tikiti moja limekuwa
likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti dogo mpaka 3000 kwa tikiti kubwa katika masoko.
Mavuno
Mavuno
ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti pia hutofautiana katika mavuno kulingana na
aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya
TANI
15-36 kwa hekta moja